Home Soka Kumekucha Msimbazi

Kumekucha Msimbazi

by Sports Leo
0 comments

Timu ya Simba sc inatarajiwa kuingia rasmi kambini siku ya leo katika hoteli  ya kifahari Sea Escape jijini Dar es salaam kujiandaa na msimu mpya wa ligi kuu na michuano ya kimataifa.

Kambi hiyo ya awali itakua na mambo mbalimbali ikiwemo kugawa vifaa vya mazoezi kwa wachezaji na benchi la ufundi watakavyotumia kwa msimu huu huku kesho wachezaji watapewa semina elekezi ili kupandisha morali ya timu kwa ujumla ambapo wachezaji watafundishwa miiko na tamaduni pamoja na historia ya klabu hiyo.

KUPAA BONDENI JUMATATU

banner

Pia timu hiyo itasafiri kuelekea nchini Afrika kusini kuweka kambi maalumu ya maandalizi ya msimu mpya(Pre-Seasons) kwa ajili ya msimu mpya wa ligi na michuano ya kimataifa ambapo timu hiyo ilifanikiwa kufika hatua ya robo fainali.

Ikumbuwe timu hiyo baada ya kufanya vizuri katika michuano hiyo mikubwa afrika itaanzia katika hatua ya kwanza na ikishinda itaingia katika makundi moja kwa moja na kama ikipoteza itacheza michezo ya mtoano ili kuingia makundi ya kombe la shirikisho.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited