Jose Mourinho ameithibitisha dunia kuwa yeye ni zaidi ya kocha baada ya kufanikiwa kuiongoza Tottenham kuibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Westham united ukiwa na mchezo wa kwanza kwa kocha huyo tangu atangazwe kocha mpya wa timu hiyo akichukua nafasi ya Mouricio Pochetino.
Son alikua wa kwanza kuipatia bao Tottenham dakika ya 39 huku bao la pili likipachikwa na Lucas Moura dakika ya 43 na kufanya timu hiyo kwenda mapumziko ikiwa inaongoza.
Kipindi cha pili Harry Kane alifanikiwa kufikisha mabao saba baada ya kufunga bao la tatu dakika ya 49 na kuhakikisha pointi tatu kwa Mourinho baada ya Spurs kuwa na ushindi wa kusuasua siku za karibuni.
West Ham ilizinduka dakika ya 73 na kupachika bao lao la kwanza kupitia kwa Michail Antonio kabla ya lile la pili kupachikwa dakika ya 90+6 na Angelo Ogbonna.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Ushindi huo unaifanya Tottenham Hotspur kuwa nafasi ya 9 ikishinda mchezo wake wa nne na inafikisha jumla ya pointi 17 kwenye msimamo wa Ligi Kuu England