Home Soka Lamine Moro Amerudi

Lamine Moro Amerudi

by Sports Leo
0 comments

Nahodha wa Yanga, Lamine Moro amesema afya yake imeimarika na mashabiki wa timu hiyo watarajie kumuona kwenye ubora wake wakati michezo ya Ligi Kuu kwa timu yake itakapoendelea.

Moro alikosa michezo minne ya mwisho ya kumalizia ngwe ya kwanza baada ya kwenda kwao kutibiwa majeraha ya mguu aliyopata kwenye michezo ya ligi.

Ligi hiyo ngwe ya pili inatarajiwa kuendelea Februari 13 baada ya kusimama kwa muda kupisha michuano ya kombe la Mapinduzi na ya kimataifa.

banner

“Kwa sasa ni mzima wa afya njema na nipo tayari kuitumikia timu yangu, unajua nilikuwa kwenye kipindi kigumu nilikuwa nasumbuliwa na majeraha sehemu ya mguu lakini baada ya kupata matibabu naona nipo vizuri na madaktari wameniruhusu kufanya mazoezi,” alisema.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited