Mastaa wa klabu ya Yanga sc wataikosa michuano ya kombe la mapinduzi kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kukabiliwa na michuano ya kimataifa pamoja na matatizo ya kifamilia.
Nahodha Lamine Moro yeye amepewa ruhusa kwenda kuonana na familia yake baada ya kutosafiri kwa muda mrefu sababu ya mipaka ya kimataifa kufungwa hivyo uongozi umeona ni wakati muafaka kujumuika na familia yake nchini Ghana.
Mastaa Deus Kaseke,Feisal Salum,Ditram Nchimbi,Farid Musa,Bakari Mwamnyeto na Yassin Mustapha wanakabiliwa na mechi za kirafiki za kimataifa wakiwa na kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania hivyo wataikosa michuano hiyo ama watajiunga wakiwa wamechelewa.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.