Home Soka Lamine,Kazimoto Wafungiwa

Lamine,Kazimoto Wafungiwa

by Sports Leo
0 comments

Beki wa Lamine Moro amefungiwa mechi tatu na kupigwa faini ya shilingi laki tano (500,000/-) kwa kosa la kumkanyaga mchezaji wa JKT Tanzania, Mwinyi Kazimoto ambaye naye amefungiwa mechi mbili kwa kosa la kusababisha vurugu kwenye mchezo wao uliopigwa Juni 17, 2020 kwenye Uwanja wa Jamhuri Dodoma.

Pia Taarifa iliyotolewa na Bodi ya Ligi imeeleza kuwa , Kamati ya Saa 72 pia imepokea malalamiko ya Azam Fc kuhusu uamuzi uliofanywa katika mchezo wao dhidi ya Yanga sc malalamiko ambayo yamepelekwa kwenye Kamati ya waamuzi.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited