Kuelekea mchezo wa ligi kuu dhidi ya Polisi Tanzania klabu ya Yanga sc itawakosa wachezaji wake mahiri Lamie Moro na Michael Sarpong baada ya kutokana na sababu mbalimbali.
Mkuu wa idara ya habari ya klabu hiyo Hassan Bumbuli amethibitisha kukosekana kwa wachezaji hao kutokana na Sarpong kusumbuliwa na majeraha huku Moro akitumikia adhabu ya kadi tatu za njano.
Hata hivyo klabu hiyo imepata nafuu baada ya kurejea kwa mshambuliaji Ditram Nchimbi ambaye alikosekana mchezo uliopita dhidi ya Coastal Union ambao timu hiyo ilipoteza kwa mabao 2-1.