Home Soka Liverpool kumng’oa Bellingham Dortmund

Liverpool kumng’oa Bellingham Dortmund

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya soka ya Liverpool imeanza mchakato wa kumsajili kiundo wa klabu ya Borussia Dortmund ya Ujerumani Jude Bellingham anayethaminishwa na klabu yake kwa dau la euro milioni 80.

Bellingham alijiunga na Dortmund majira ya joto 2020 akitokea Birmigham ya Uingereza kwa euro milioni 22 kwa mkataba wa miaka mitano.

Kiungo huyo alikua akitakiwa kwa udi na uvumbi na Manchester United kabla ya kuichagua Dortmund na Liverpool wanamuona kinda huyo kama mbadala wa kiungo Gini Wanaldum alyetimkia PSG baada ya mkataba wake kuisha ndani ya majogoo hao wa Marseyside.

banner

Mchezaji huyo amekuwa katika kiwango kizuri tangu ajiunge na Dortmund na mara kadhaa amekuwa akisifiwa na makocha wakubwa kama Guadiola juu ya uwezo na haiba yake ya uchezaji hali inayovivutia vilabu vikubwa Ulaya kama Liverpool pamoja na kujumuishwa kwenye kikosi cha gtimu ya taifa ya England kilichoshiriki Euro 2020.

Thamani ya mchezaji huenda ikawa kikwazo kwa Liverpool kutokana na Dortmund kutokuwa na masihara katika biashara ya kuuza wachezaji.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited