Imeripotiwa kuwa Klabu ya Strømsgodset inayoshiriki Ligi Kuu nchini Norway inahitaji saini ya mshambuliaji wa Simba, Mnigeria Lokosa Junior.
Lokosa mwenye umri wa miaka 27, ana mkataba wa miezi SITA na Simba SC, Lakini klabu hiyo imeonyesha nia ya kununua kandarasi hiyo.
Rekodi zinaonyesha kuwa Lokosa akiwa Kano Pillars ya kwao Nigeria ndani ya msimu wake wa kwanza tu, alicheza mechi 14 na kutupia nyavuni mabao matano hiyo ikiwa mwaka 2017.
Msimu uliofuata, 2018 aliendelea kuuwasha moto na kufunga mabao 14 katika michezo 15 tu.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Cc:Shaffihdauda