Beki wa kushoto wa klabu ya Yanga sc Joyce Lomalisa anatarajiwa kuukosa mchezo wa tatu wa hatua ya makundi ya kombe la klabu bingwa barani Afrika dhidi ya Medeama Fc baada ya kushindwa kupona majeraha.
Beki huyo aliumia katika mchezo wa sare ya 1-1 dhidi ya Al Ahly baada ya kukanyagwa na Percy Tau ambapo alitolewa nje kwa matibabu zaidi na nafasi yake kuchukuliwa na Nickson Kibabage ambapo sasa ripoti ya madaktari wa klabu hiyo imeonyesha kuwa bado hajapona.
Kocha Miguel Gamondi sasa inampasa kumuanzisha mmoja kati ya Nickson Kibabage,Farid Musa ama Kibwana Shomari katika eneo hilo ili kuziba nafasi ya Lomalisa anayesifika kwa kupiga krosi nzuri za ushindi.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Tayari msafara wa kikosi hicho umeanza safari kuelekea nchini Ghana huku staa huyo akisalia nchini kwa ajili ya kuendelea na matibabu zaidi.