Mshambuliaji wa kimataifa wa Ubelgiji Romelu Lukaku amejiunga rasmi na mabingwa wa soka barani Ulaya klabu ya Chelsea kwa mkataba wa miaka mitano akitokea Inter Milan ya Italia.
Lukaku amerejea darajani kwa ada ya paundi milioni 97.5 baada ya miaka saba.
Straika huyo ameifungia Inter Milan mabao 64 katika michezo 95 na anakwenda Chelsea kufanya kazi moja ya kutupia mipira nyavuni na huenda ujio wake ukapelekea kuuzwa kwa straika Muingereza Tammy Abraham anayehusishwa kujiunga na As Roma ama Arsenal.