Nahodha wa Namungo Reliant Lusajo ameiweka njia panda klabu yake ya Namungo Fc baada ya kugoma kusaini mkataba mpya huku akitoa masharti ya kutimizwa.
Klabu hiyo ilifanya mazungumzo na meneja wa mchezaji huyo lakini walishindwa kufikia muafaka hivyo kuleta sintofahamu ukizingatia timu kama Yanga sc na Simba sc zinamnyemelea staa huyo mwenye mabao 11 ya ligi kuu.
Hata hivyo taarifa za ndani ya Namungo zinasema tayari kocha Hitimana Thierry ameshapata mbadala wa mshambuliaji huyo pamoja na Bigirimana Blaise kama wakiamua kuondoka mwishoni mwa msimu ambapo mikataba yao itakua inafikia mwishoni.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.