Kocha mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck amesema tayari amejulishwa na viongozi wa klabu hiyo kwamba kila kitu juu ya Lwanga kimekamilika.
Kocha huyo amesema kutokana na taarifa hizo ndio maana walisafiri naye kwenye mechi dhidi ya FC Platinum na kwamba alishindwa kumtumia kwa vile alipatwa na mafua na kumpumzisha na hata katika mechi yao ya Ligi dhidi ya Ihefu hakumtumia, ila amesema;
“Kama hali yake itakuwa sawa na atafanya mazoezi vizuri nimepanga kuanza kumtumia katika mchezo wa marudiano dhidi ya Platinum”
.