134
Azam FC imefanikiwa kuingia mkataba mpya wa miaka miwili na kiungo mshambuliaji, Ayoub Lyanga.
Zoezi la kuingia mkataba huo baina mchezaji na klabu huyo limesimamiwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa timu hiyo Abdulkarim Amin ‘Popat’.
Lyanga aliyejiunga na Azam Fc msimu huu akitokea Coastal Union, ataendelea kusalia ndani ya viunga vya Azam Complex hadi mwaka 2024.
Ukiwa ni msimu wake wa kwanza ndani ya Azam FC, Lyanga amefanikiwa kuchangia mabao 10 kwenye mashindano yote hadi sasa msimu huu.
Takwimu zinaonyesha kuwa, Lyanga amefunga mabao saba na kutoa pasi mbili za mwisho za mabao kwenye Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL), huku akitupia moja katika michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports (ASFC).
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.