Kiungo Mshambuliaji Balama Mapinduzi amekamilisha awamu ya kwanza ya matibabu baada ya kukamilisha vipimo sasa jopo la madaktari litaamua namna ya matibabu yake kuanzia kesho
Awamu ya kwanza ilikuwa ni vipimo vya aina tatu , ambavyo vimekamilika , kinachofuata sasa ni Madaktari kuona matibabu gani yanafaa kwa Balama baada ya kujiridhisha na majibu ya vipimo , ” amesema Afisa Habari wa Yanga , Hassan Bumbuli
Amesema vipimo vyote vimekamilika na madaktari wamegundua kwamba mfupa uliunga vibaya hali ambayo ilikuwa ikisababisha maumivu kwenye mguu akifanya mazoezi.
Balama aliumia mazoezini wakati klabu yake ikijiandaa na mazoezi kujiandaa na mchezo dhidi ya Simba sc katika uwanja wa chuo cha Sheria jijini Dar es salaam.