Klabu ya Manchester City wametwaa ubingwa wa ligi kuu nchini Uingereza kwa mara ya saba huku ikitwaa taji hilo mara tatu ndani ya miaka mitano chini ya kocha Pep Guadiola.
Licha ushindi wa klabu ya Manchester City ambao walijihakikishia muda mrefu,mchuano mkubwa ulikua katika nafasi za kufuzu hatua ya michuano ya klabu bingwa barani ulaya ambapo ManUtd,Chelsea,Liverpool,Tottenham Fc na Leicester City walikua wanawania nafasi nne zilizobaki ili kufuzu michuano hiyo mikubwa barani ulaya.
Baada ya mechi ya mwisho za ligi kuu hapo jana sasa ni rasmi Chelsea imeungana na Man Utd,Liverpool,Man City kufuzu michuano hiyo huku Tottenham na Leicester City zikifuzu michuano ya Europa.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.