Klabu ya Manchester United imeendelea kung’ang’ania kileleni mwa msimamo wa ligi kuu nchini Uingereza baada ya jana kuifunga timu ya Fulham mabao 2-1 katika mchezo wa ligi hiyo uliofanyika katika uwanja wa Craven Cottage.
Wenyeji walipata bao la mapema dakika ya 5 kutoka kwa Ademola Lookman aliyevunja mtego wa kuotea na kupiga shuti kali lililomshinda kipa David De Gea.
Edso Cavani aliunganisha mpira uliotemwa na kipa wa Fulham na kusawazisha bao hilo huku juhudi binafsi za Paul Pogba aliyepiga shuti kali lililomshinda golikipa wa Fulham na kuipa united ushindi ulioifanya ibaki kileleni na alama 40.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.