Taarifa kutoka nchini Sudan zinadai kocha mkuu wa klabu ya El Merrekh amemuomba tajiri wa klabu hiyo kumsajili golikipa wa klabu ya Simba sc Aishi Manula.
Kocha huyo amevutiwa na uwezo wa kipa huyo tegemea nchini pamoja na timu ya Taifa ya Tanzania kutokana na uhodari wake wa kuokoa michomo uliosaidia kuifanya klabu ya Simba sc kuongoza kundi lake katika michuano ya klabu bingwa barani Afrika hali iliyomfanya kutoruhusu goli mpaka sasa.
Inadaiwa klabu hiyo inajiandaa kutoka kiasi cha dola laki moja kama ofa ya awali kwa klabu ya Simba sc ili kumnasa kipa huyo.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.