Klabu ya Yanga sc inatarajiwa kusaini wachezaji wa kigeni wapya watano ili kuongeza nguvu katika kikosi hicho kuusaka ubingwa wa ligi kuu msimu ujao.
Mpaka sasa klabu hiyo ina wachezaji wa kigeni tisa huku ikiwa tayari imeachana na Carlos Carlinhos na ina mpango wa kutema wengine watano wakiongozwa na Fiston Abdulrazack pamoja na Michael Sarpong ili kutoa nafasi kwa wengine watano kuingia kikosini.
Inatajwa tayari timu hiyo imemsajili Djuma Shabani huku ikisaka beki wa kati mbadala wa Lamine Moro ambaye majeraha na utovu wa nidhamu vinamponza huku mazungumzo na Heritier Makambo yakiwa yameanza kuongeza nguvu katika upatikanaji wa mabao na kiungo mshambuliaji inadaiwa tayari usajili unaendelea na anatokea nchini Kongo.