Wachezaji wa klabu ya Chelsea kwa pamoja wamekubali kukatawa asilimia 10 ya mshahara kuanzia mwezi mpaka mwezi Septemba kama njia ya kusaidia klabu kupambana na mdororo wa mapato kutokana na Virusi vya Corona.
Mastaa hao kwa pamoja walifikia muafaka huo baada ya kuwasiliana kupitia mtandao wa Whatsup wa wachezaji hao ambapo waliongozwa na nahodha Cezar Azpilicueta kupitisha wazo hilo.
Chelsea inakua timu ya kwanza kupitisha mfumo huo ambao upo tofauti na Arsenal watakaokatwa asilimia 12.5 lakini zitakuja kufidishiwa kama bonansi.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.