Klabu ya Yanga sc itaanza kupokea mastaa wapya kwa ajili ya msimu kuanzia kesho jumatatu baada ya ligi kuu kumalizika rasmi hii leo.
Mastaa hao wanaokuja kusaini mikataba ya kukipiga klabuni hapo wataanza kuwasili nchini kwa ushirikiano mkubwa kati ya kamati ya usajili ya klabu hiyo pamoja na kampuni ya Gsm iliyojitolea kuisaidia klabu hiyo ambayo ni mabingwa wa kihistoria nchini.
Sogne Yacouba ni moja ya mastaa wanaotajwa kuwasili nchini akitokea nchini Ghana baada ya kumaliza mkataba na klabu ya Asante Katoko aliyokua akiichezea na sasa ni suala muda tu kabla ya kuja kukipiga jangwani.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.