Home Soka Mbabe wa Simba sc Atimuliwa Kaizer Chiefs

Mbabe wa Simba sc Atimuliwa Kaizer Chiefs

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Kaizer Chief imethibitisha kumfungashia vilago kocha mkuu Gavin Hunt licha ya kufanikiwa kuivusha timu mpaka hatua ya nusu fainali ya michuano ya klabu bingwa Afrika baada ya kuifunga Simba sc kwa jumla ya mabao 4-3 katika michezo yote miwili.

Makocha wasaidizi Arthur Zwane na Dillon Sheppard watakaimu nafasi hiyo hadi kocha mkuu mpya atakapoteuliwa huku mfululizo wa matokeo yasiyoridhisha na kiwango kibovu cha timu ikiwa kimechangia kutimuliwa kwake.

Takwimu za kocha huyo tangu ajiunge na klabu hiyo katika kipindi cha miezi nane ni alihudumu katika michezo 44 akishinda 12 sare 15 na kufungwa 15 huku akiiacha klabu hiyo katika nafasi ya 11 ya ligi kuu Afrika Kusini.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited