Home Soka Metacha aachana na wakala wake

Metacha aachana na wakala wake

by Sports Leo
0 comments

Mlinda  mlango wa Polisi Tanzania Metacha Mnata ametangaza rasmi kuachana na wakala wake wa muda mrefu Jemedari Said hii leo kupitia ukurasa wake rasmi wa mtandao wa kijamii wa Instagram.

Mchezaji huyo amechukua uamuzi huo kwa kile kinachosemekana huenda akarejea katika klabu yake ya zamani Young Africans kipindi hiki cha dirisha dogo la usajili ili kuwa mbadala wa mlinda mlango namba moja Diarra anayekwenda kushiriki michuano ya kombe la mataifa Afrika nchin Cameroon akiwa na timu ya taifa ya Mali.

Moja ya masharti aliyopewa Metacha ili kurudi Yanga ni pamoja na kuachana na meneja Jemedari ambaye siku za hivi karibuni amekuwa hana maelewano mazuri na viongozi wa klabu hiyo hali wanayoiona ndiyo iliyochangia mlinda mlango huyo kuondoka mwishoni mwa msimu uliopita.

banner

Kupitia posti aliyoweka instagram Metacha aliandika ”nachukua nafasi hii kukushukuru kwa muda wote na kuwa pamoja katika maisha yangu,tuliachana muda mrefu lakini ilibaki utaratibu na wakati umefika wa kukushukuru sana na kila la kheri katika ufanisi wako Jmedari”.

Komenti ya msemaji wa Yanga Haji Manara imechagiza zaidi kuwa huenda ni kweli Metacha anarejea Jangwani,baada ya posti hiyo Manara alikomenti ”Bravoooo kipa wa mpira,,na inshaalah utafanikiwa zaidi katika career yako”.Ikumbukwe pia Manara amekuwa hana mahusiano mazuri na Jemedari Said kiasi cha kutupiana maneno mara kwa mara.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited