Kocha wa Kagera Sugar Mecky Mexime ameukubali uwezo wa kikosi cha Simba baada ya kufungwa mabao 3-0 katika uwanja wa nyumbani wa Kaitaba uliopo mjini Bukoba mkoani Kagera mchezo uliofanyika jana.
Awali kocha huyo alijitapa atawafunga Simba sc akiringia rekodi yake ya msimu uliopita alopowafunga wanamsimbazi hao mechi zote za nyumbani na ugenini.
Tambo hizo zilikoma baada ya dakika 90 za mchezo huo kufuatia mabao ya Meddie Kagere aliyefunga mawili na Mohamed Hussein yaliyoipa pointi tatu simba ugenini.
“Simba ni timu bora sio tu ndani ya nchi bali hata Afrika ukitaja timu bora nne simba itakuwemo,lSisi tulifanya makosa kadhaa na wenzetu wameyatumia”.Alisema Mexime
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Kagera ilikua imeshinda mechi zote za awali na kuwafanya kuongoza ligi kwa kuwa na pointi tisa kabla ya jana kukubali kipigo hicho.