Licha ya kucheza pungufu kwa zaidi ya dakika 45 klabu ya Prisons imefanikiwa kuibana klabu ya Simba sc na kufanikiwa kugawana alama moja moja katika mchezo wa ligi kuu Tanzania bara uliofanyika uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es salaam.
Jumanne Elfadhiri alipewa kadi nyekundu ya moja kwa moja baada ya kumpiga teke Mzamiru Yassin mwishoni mwa kipindi cha kwanza huku Salum Kimenya aliipatia Prisons bao mwanzoni mwa kipindi cha pili baada ya kupiga faulo iliyovuka ukuta na kumshinda golikipa Aishi Manula.
Jitihada za Benard Morrison na Luis Miqquisone zilizaa bao katika dakika ya mwisho ya dakika tano za nyongeza na kufanya mchezo umalizike kwa 1-1.