Licha ya kuwa na matatizo ya kinidhamu ya mara kwa mara kiasi cha kuitwa katika kamati ya nidhamu ya klabu ya Simba sc,Inadaiwa kuwa kiungo wa klabu hiyo Jonas Mkude bado yupo sana klabuni hapo.
Hivi majuzi kamati ya nidhamu ya klabu hiyo iliamuru kuwa staa huyo aende kupimwa akili katika Hospitali ya taifa ya Muhimbili kutokana na mfululizo wa matukio hayo ili kujua aina ya uamuzi wa kuchukua kwa kamati hiyo baada ya kupata ripoti ya madaktari.
Mkuu wa kamati hiyo Seleman Kova amethibitisha kuwa staa huyo ana mkataba na klabu hiyo hivyo hawafanyi kwa lengo la kutaka kumkomoa ama kumuacha mchezaji huyo.
“Kuna watu nimeskia katika maoni yao wanafikiria labda mkataba wa Mkude unakaribia kuisha kwa hiyo Simba au sisi tunatumika kumkomoa mchezaji.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
“Nimeangalia mkataba wa Mkude bado ni mbichi kabisa, ni mchezaji anayependwa na kila Mwanasimba lakini linapotokea tatizo ni lazima lishughukikiwe.Alisema Kamanda Kova aliyewahi kuwa mkuu wa polisi mkoa wa Dar es saalam.