Tajiri wa klabu ya Simba sc Mohamed Dewji amechagulia kuwa mshauri wa masuala ya uchumi na uwekezaji wa Rais wa Afrika ya Kusini Cyril Ramaphosa ambapo atatumikia nafasi hiyo kwa kipindi cha miaka mitano.
Rais huyo amelazimika kumteua mfanyabiashara na bilionea huyo kijana nchini kutokana na mafanikio yake ya kuikuza chapa ya kampuni ya Metl pamoja na kupanua wigo wa biashara wa makampuni hayo kimtaifa.
Mo dewji ametajwa na jarida la kimataifa la Forbes kama tajiri kijana huku akiwa tajiri wa 13 katika matajiri 18 waliopo barani Afrika.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.