Mwekezaji wa klabu ya soka ya Simba Mohamed Dewji ameachia rasmi uenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi wa klabu hiyo yenye maskani yake mitaa ya Msimbazi jijini Dar es salaam na kumteua Salim Abdallah Try again kushika wadhifa huo
Hayo yameelezwa leo na Dewji mwenyewe kwenye mkutano na waandishi wa habari akitaja kuwa ugumu wa ratiba zake za kiofisi zimepelekea yeye kujivua madaraka hayo.
Awali kulikuwa na tetesi kuwa Bilionea huyo angejitoa kuwekeza katika klabu lakini kupitia mkutano huo amekanusha taarifa na kubainisha kuwa bado yumo sana Simba na amefanya hivyo ili kupunguza tu majukumu hivyo yeye atabaki kuwa mwekezaji tu na si vinginevyo.
Taarifa zisizo rasmi zinadai kuwa kwa mujibu wa taratibu za tume ya ushindani nchini,mwekezaji anayewekeza katika taasisi ya umma hatakiwi kuwa na nyazifa mbili na ndio sababu nyingine inayotajwa kumwondoa bilionea huyo madarakani.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Mo Dewji ametumia ukurasa wake wa Instagram kuweka video akisema kuwa bado yupo sana Simba hivyo wanachama na mashabiki wa timu hiyo wasiwe na wasiwasi juu ya kujiengua kwake nafasi hiyo.