Mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Yanga sc David Molinga ‘Falcao’amejiunga na Namungo Fc inayoshiriki ligi kuu nchini baada ya kumalizana na timu ya Zesco United nayoshiriki ligi kuu ya nchini Zambia.
Awali kabla ya kujiunga na Zesco United Molinga alicheza Yanga sc na kuwa kipenzi cha mashabiki akifunga mabao 12 kwa msimu wa ligi kuu 2019/2020 lakini Yanga sc waliamua kumuacha na kusajili majembe mapya wakina Michael Sarpong na Yacouba Sogne.
Inadaiwa Namungo Fc imekamilisha usajili wa Molinga ambae atakuja kuungana na Obrey Chilwa na Steven Sey pamoja na Bigirimana Blaize katika safu ya ushambuliaji klabuni hapo.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.