Home Soka Molinga Azua Sekeseke Yanga

Molinga Azua Sekeseke Yanga

by Dennis Msotwa
0 comments

Mshambuliaji wa klabu ya Yanga David Molinga amegoma kusafiri na timu kwenda mkoani Shinyanga kucheza na Mwadui kwa kudai kuwa timu hiyo inapendelea baadhi ya wachezaji.

Molinga amelalamika kwa madai ya kuwa kocha Bonifasi Mkwasa anawapendelea baadhi ya mastaa katika timu hiyo wakiwemo Haruna Niyonzima na Benard Morrison kwa madai ya kuwapa nafasi mara kwa mara hata kama hawajafanya mazoezi na timu.

Staa huyo aliyebakiza mkataba wa miaka miwili katika klabu hiyo amedai kwamba mkataba wake utakapoisha ataondoka klabuni hapo kwa kuwa anaona hahitajiki.

banner

Yanga imesafiri leo kuwafata Mwadui Fc mkoani Shinyanga kwa kutumia usafiri wa basi huku ikiacha baadhi ya mastaa kwa sababu mbalimbali.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited