Timu ya Taifa ya Morocco maarufu kama simba wa Atlas wamefanikiwa kusonga mbele katika hatua ya mtoano ya michuano ya kombe la Mataifa Afrika(AFCON) linaloendelea nchini Cameroon.
Morocco wamefanikiwa baada ya kuifunga timu ya Taifa ya Visiwa vya Comoro kwa mabao 2-0 na kufikia alama sita kileleni mwa msimamo wa kundi C na hivyo kujihakikishia nafasi.
Magoli kutoka kwa washambuliaji Selim Amallah dakika ya 16 na Zakaria Aboukhlal dakika ya 89 yalitosha kuwapa ushindi muhimu huku mshambuliaji Yousuf En Nesyri akikosa mkwaju wa penati dakika ya 83.
Kwa upande mwingine timu ya Taifa ya Ghana imeshindwa kupata ushindi katika mchezo wake wa pili katika kundi hilo baada ya sare ya 1-1 na Gabon na kuwaweka katika nafasi finyu ya kufuzu hatua ya mtoano.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Nayo timu ya Taifa ya Malawi anayochezea mchezaji wa Simba sc Peter Banda imeapa ushindi wa 2-0 dhidi ya Zimbabwe katika mchezo wa kundi B.