Kiungo Mshambuliaji wa Simba SC Benard Morrison ataukosa mchezo wa kesho wa ligi kuu Vodacom Tanzania Bara (VPL) ambapo Simba itawakabili Kagera Sugar mchezo utakaopigwa katika dimba la Kaitaba mkoani Kagera, Morrison atakosa mchezo huo kutokana na kuwa na kadi tatu (3) za njano.
Hata hivyo mchezaji huyo yupo kwenye hatihati ya kufungiwa na shirikisho la soka nchini Tff baada ya kipande cha video kuonyesha kuwa alimbugudhi mwamuzi wa pembeni katika mchezo dhidi ya Simba sc na Mwadui katika uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.