Mastaa tegemeo katika kikosi cha Yanga Kipa Metacha Mnata na Winga Benard Morrison wameachwa katika kikosi cha timu hiyo kilichoondoka leo kuelekea Shinyanga kuwavaa Mwadui fc.
Yanga imeondoka leo jijini Dar es salaam kwa usafiri wa basi na kuwaacha mastaa hao kwa sababu mbalimbali ambapo Morrison alichelewa msafara wa timu huku Metacha akiwa na ruhusa maalumu kutoka kwa uongozi kushughulikia matatizo ya kifamilia.
Taarifa kutoka Yanga zinadai mastaa hao wataungana na timu hiyo kesho ambapo wataondoka kwa ndege wakiwa na kocha Luc Eymael anayetarajiwa kuwasili leo saa saba mchana.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.