Klabu ya Tottenham imemfuta kazi mkufunzi wake mkuu Jose Mourinho baada ya kudumu nae kwa miezi 17 tangu ajiunge mwaka 2019 akisaidia timu kumaliza nafasi ya sita ya ligi kuu msimu uliopita.
Pamoja na Mourinho,Pia wasaidizi wake wote wametimuliwa klabuni hapo wakiwemo kocha ya viungo,makipa na kocha wa kikosi cha kwanza wakiiachia timu hiyo kibarua kizito dhidi ya Man city katika mchezo wa fainali ya Carabao Cup tarehe 25 mwezi huu.
Mourinho amevuna alama mbili pekee katika mechi tatu za ligi kuu nchini Uingereza huku akitolewa katika michuano ya Europa huku akifungwa michezo kumi katika msimu huu tangu aanze kufundisha soka.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.