Kuna mpasuko mkubwa katika klabu ya Barcelona fc baada ya wajumbe sita wa bodi ya wakurugenzi kujiuzuru ndani ya muda mfupi huku wakikosoa uongozi wa Rais wa klabu hiyo Josep Maria Bartomeu.
Emili Rousaud na Enrique Tombas ambao ni kati ya makamu wa Rais wanne wa klabu hiyo wamejiuzuru sambamba na madarkta wanne wa klabu hiyo Silvio Elias, Josep Pont, Jordi Calsamiglia na Maria Teixidor.
Inadaiwa vigogo hao wamechukizwa baada ya kugundua klabu ilishirikiana na mtandao wa kijamii wa unaoitwa Barcagate ambao uliwashambulia wachezaji wa klabu hiyo pia janga la corona pamoja na uchaguzi mkuu wa klabu hiyo vikitajwa.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.