Beki wa klabu ya Yanga sc Abdala Shaibu ”Ninja”leo anatarajiwa kusafiri kuungana na timun hiyo jijini Mbeya baada ya kutokusafiri jana kufuatia kupatwa na msiba wa dada yake siku ya juzi.
Beki huyo katili alipata taarifa za msiba wa dada yake wakati timu ikiwa katika maandalizi ya kuwavaa Azam Fc na ndipo alipoamua kumaliza mechi kisha kuhudhuria mazishi ya dada yake yaliyofanyika jana.
Hata hivyo baada ya msafara wa klabu hiyo kusafiri hapo jana kuelekea jijini Mbeya ambapo wataweka kituo kabla ya kuelekea mjini Sumbawanga kuwavaa Prisons siku ya ijumaa jioni ambapo beki huyo atakuwepo baada ya kukamilisha taratibu zote za safari na leo jioni ataungana na wenzake mazoezini.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.