Mwamuzi Abubakar Mturo amefungiwa miezi mitatu(3) kwa kosa la kushindwa kumudu mchezo katika mechi iliyochezwa Februari 05,2020 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Kanuni namba 39(1) ya Ligi Kuu Kuhusu Udhibiti wa Waamuzi baada ya kuvurunda katika mchezo kati ya Yanga na Lipuli ambapo alisababisha sintofahamu baada ya kuamuru kona katika mpira ambao haukutoka nje.