Klabu ya Namungo Fc imesafiri alfajiri ya leo kuelekea nchini Zambia kuivaa klabu ya Nkana Fc katika mchezo wa marudiano hatua ya makundi utakaofanyika nchini humo.
Katika mchezo wa awali uliofanyika nchini Tanzania Namungo ilikubali kichapo cha 1-0 huku wakibaki katika nafasi ya nne katika msimamo wa kundi D huku Nkana wakiwa nafasi ya tatu chini ya Raja Casablanca na Pyramids Fc zote ziliifunga Namungo Fc.
Hemmed Moroco ambaye ni kocha wa Namungo Fc amesema kwamba matokeo hayo ni sababu ya kutokua na uzoefu pamoja na kutotumia nafasi vizuri.