Site icon Sports Leo

Nchimbi Aongoza Mauaji ya Gwambina

Klabu ya Yanga sc imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Gwambina katika mchezo wa ligi kuu nchini uliomalizika katika uwanja wa Mkapa Dar es salaam.

Mabao ya Ditram Nchimbi,Bakari Mwamnyeto na Saido Ntibanzokiza yalitosha kutuma salamu kwa wapinzani kuwa Yanga sc bado haijakata tamaa ya kubeba ubingwa wa ligi kuu nchini.

Awali katika michezo iliyopita dhidi ya Kmc na Biashara united timu hiyo ilifanikiwa kuvuna alama nne hivyo ushindi dhidi ya Gwambina unaifanya timu hiyo kufikisha alama 55 katika michezo 26 ikiwa kileleni mwa msimamo.

Exit mobile version