Kocha Mkuu wa timu ya soka ya taifa ‘Taifa Stars’, Ettiene Ndayiragije amesema walipambana kwa uwezo wao ili kuhakikisha wanasonga hatua ya robo fainali ya michuano ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani (Chan) ila bahati haikuwa ya kwao.
“Tunashukuru Mungu tumemaliza salama, wachezaji wamejitahidi kupambana ila bahati haikuwa yetu, kuna mambo mengi tumeona, mwamuzi alituvunja moyo kwa kuwapa penalti wapinzani na mengine.
Ndayiragije amesema licha ya kushindwa kusonga mbele kikosi chake kilionesha kuimarika kutoka mechi moja kwenda nyingine na ni timu inayokua.
Naye Kipa wa Taifa Stars, Aishi Manula alisema walitamani kushinda na kusonga mbele ila imekuwa tofauti, wanashukuru Mungu kwa yote na ana amini wamejifunza na watafanya vizuri wakati mwingine.
Cc:Kibezedon