Home Soka Ndumbaro Ateta na Mastaa Stars

Ndumbaro Ateta na Mastaa Stars

by Sports Leo
0 comments

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amefanya mazungumzo maalumu na kikosi cha timu ya Taifa (Taifa Stars) kilichoweka kambi katika Jiji la San Pedro nchini Ivory Coast kujiandaa na mchezo wa kwanza wa mashindano ya AFCON 2023 dhidi ya Morocco.

Mhe. Ndumbaro amezungumza na wachezaji hao mara baada ya kushuhudia mazoezi na utayari wa kikosi hicho kuelekea mchezo wao na Timu ya Taifa ya Morocco utakaopigwa jijini humo Januari 17, 2024.

banner

Baada ya mazungumzo yaliyodumu kwa muda wa takribani saa mbili, Waziri Dkt. Damas Ndumbaro amesema ameridhishwa na maandalizi ya kikosi hicho, Ari na morali ya wachezaji na benchi la ufundi ambayo inatoa picha nzuri ya kufanya vizuri katika kundi F la michuano hiyo.

Kikao hicho kimehudhuriwa pia na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF), Bw. Wallace Karia, Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFF) ambaye pia ni Mkuu wa msafara wa timu Bw. Suleiman Mahamoud Jabir.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited