Home Soka Neymar Aikataa Psg

Neymar Aikataa Psg

by Sports Leo
0 comments

Mshambualiaji wa Brazil Neymar amemwambia mkurugenzi wa timu ya Paris st German(PSG) kuwa anataka kuondoka klabuni hapo katika majira haya ya kiangazi huku ikitajwa kuwa mchezaji huyo anataka kurejea Barcelona.

Mchezaji huyo alichelewa kujiunga na kambi ya maandalizi ya msimu mpya lakini imeripotiwa baada ya kufika kambini alimwambia mkurugenzi wa michezo wa klabu hiyo Leonardo kuwa anataka kuondoka jijini Paris japo mkurugenzi huyo alijaribu kumshawishi staa huyo kubadili maamuzi yake huku akificha wapi anataka kuelekea.

banner

Imefahamika kuwa Barcelona wako tayari kutoa pesa na mchezaji kwa ajili ya kukamilisha usajili wa mchezaji huyo baada ya kuwa wamekamilisha usajili wa Antoine Griezman kwa dau la paundi 108 milioni.

Neymar 27 aliondoka Barcelona miaka miwili iliyopita kwa dau la rekodi la paundi 197 milioni na sasa inafahamika kuwa anataka kurejea klabuni hapo.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited