Home Soka Ni vita ya wakubwa nusu fainali carabao

Ni vita ya wakubwa nusu fainali carabao

by Sports Leo
0 comments

Hatimaye vilabu vine vitakvyoshiriki nusu fainali ya kombe la carabao vimepatikana mara baada ya michezo mingine mitatu ya robo fainali kuchezwa usiku wa kuamkia leo na kushuhudia Tottenham,Chelsea na Liverpool vikiungana na Arsenal katika hatua inayofuata.

Chelsea walikuwa darajani walipata ushindi wa 2-0 na kutinga nusu fainali yao ya tatu tangu ndani ya mwaka huu tangu kutua ka Thomas Tuchel.Goli la kujifunga kutoka kwa beki wa Sweden Pontus Jasson na lile la penati kutoka kwa Jorginho yaliwahakikishia kusonga mbele,licha ya kuwa na majeruhi kadhaa na wagonjwa wa Uviko-19.

Tottenham wamefanikiwa kutinga nusu fainali ya michuano hiyo baada ya kuwachapa West Ham 2-1 ikiwa ni nusu fainali yao ya kwanza toka mwaka 2019.Magoli ya Steven Bergwin dakika ya 29 na Lucas Moura dakika ya 34 yalitosha kuwapa ushindi vijana hao wa Antonio Conte.

banner

Liverpool walikuwa Anfield walisubiri hadi hatua za mikwaju ya penati kujua hatma yao baada ya sare ya mabao 3-3 dhidi ya Leicester City.Licha ya kuongoza 2-0 lakini vijana wa Rodgers hawakuweza kusonga mbele baada ya Liverpool kusawazisha,shujaa wa mchezo ni golikipa Kelleher aliyeokoa mikwaju miwili ya penati na kuipa ushindi timu yake.

Michezo ya nusu fainali itazikutanisha Arsenal dhidi ya Liverpool huku Chelsea wakivaana na Tottenham kati ya Januari 4 kwa mechi za awali na Januari 11 kwa mechi za marudiano.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited