33
Mshambuliaji wa Klabu ya Yanga,Saido Ntibazokinza amesema hajawahi kufuta picha zake za Yanga katika akaunti yake ya mtandao wa kijamii wa Instagram Kama inavyodaiwa na wengi kwakuwa tangu amefika nchini hajawahi kuweka taarifa yoyote katika akaunti yake Kutokana na akaunti hiyo kuwa na matatizo.
“Unajua wapo ambao tangu nimefika hapa watu wamekuwa wakifungua akaunti mbalimbali za jina langu, mimi nina akaunti moja tu ya Instagram ambayo inatiki ya bluu ina jina la Ntibazonkiza”.
“Hii akaunti sijaitumia muda mrefu kwa kuwa ilikuwa ina shida na niliposaini Yanga tu niliwaomba watu wa tehama (IT) wanisaidie kuifanyia kazi na mpaka sasa bado halijakamilika,”
“Akaunti hiyo sijaweka posti yoyote ile kwa kuwa siwezi kufanya hivyo kutokana tatizo lililotokana na wao Instagram, sasa nashangaa wanaosema nimefuta picha, sijui waliona nimeweka picha gani, kama yupo ambaye ana uhakika nimefuta picha aje nayo anionyeshe.”
“ Hizo akaunti nyingine naziangalia tu watu wanaokota picha wanaziweka wanaandika vitu vyao nigewasihi watu wasimuamini mtu huko kwa sasa sina akaunti ninayoitumia, akaunti yangu ikikaa sawa nitatoa taarifa.”
Kuhusu sakata lake la kutaka kutoka uwanjani katika mchezo dhidi ya Gwambina mara tu baada ya kufunga bao, Saido amesema hilo lilishapita na kila binadamu ana uwezo wake wa kudhibiti hasira zake.
“Napenda kuisaidia timu yangu natamani kuona Yanga inashinda mechi zake kwa urahisi, shauku hiyo ndio iliyosababisha yale kutokea. Kila binadamu ana kiwango chake cha kuhimili hasira, nina moyo.Wakati ule moyo wangu uliona ufanye kile”
“Kwasasa hayo yameisha nafurahi kuona maisha yamerudi katika utulivu, sote tunashirikiana,”