Taarifa kutoka ndani ya klabu ya Simba sc zinadai kuwa mshambuliaji Emmanuel Okwi yupo mbioni kurejea klabuni hapo baada ya kuvunja mkataba na waajiri wake timu ya Alexandria inayoshiriki ligi kuu nchini Misri.
Taarifa hizo nyeti zinadai kuwa Bilionea wa klabu ya Simba sc Mohamed Dewji “Mo” ndie aliyeshawishi kufanikisha dili hilo ili kuunda pacha hatari na straika Meddie Kagere.
Okwi aliondoka msimbazi msimu ulioisha ambapo alijiunga na klabu hiyo ya nchini Misri lakini amekua akikosa nafasi mara kwa mara.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.