Klabu ya soka ya Manchester United imethibitisha kuachana na kocha wake mkuu Ole Gunnar Solskjaer mchana huu kupitia taarifa rasmi ya klabu iliyotolewa kwenye mitandao rasmi ya timu hiyo.
Man Utd na Ole wamekubaliana kusitisha mkataba wa kocha huyo uliokuwa ukimalizika mwaka 2025 kwa heshima,huku ikimtaja na kumshukuru kwa mchango mkubwa wa kuijenga timu hiyo.
Michael Carrick ametangazwa kuwa kocha wa muda wakati ambao klabu inatafuta kocha wa mpito hadi mwisho mwa msimu huu,kabla ya kutangaza rasmi kocha mpya msimu utakapoisha.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Carrick ameomba kuendelea kusalia kwa Mike Phelan na Kieran McKenna kama sehemu ya benchi la ufundi kuelekea mchezo wa ligi ya mabingwa Ulaya dhidi ya Villareal siku ya Jumanne na ule dhidi ya Chelsea wikiendi ijayo.