Manchester united ipo katika mpango wa kumsajili kiungo mkabaji wa Leeds united Kavin Phillips baada ya kushindwa kumsajili kiungo wa West ham Declan Rice kutokana na dau kubwa lililowekwa na klabu yake.
Kavin amekuwa katika kiwango kizuri chini ya mkufunzi Marcelo Bielsa tangu kupanda kwa Leeds katika ligi kuu ya Uingereza msimu uliopita kiasi cha kumfanya kocha wa timu ya taifa Gareth Southampton kumjumuisha katika timu ya taifa na kuwa tegemeo kwenye timu hiyo.
Manchester united wamekuwa wakisaka kiungo mkabaji kwa muda mrefu baada ya Fred na McTominay kushindwa kuonesha ubora katika eneo hilo huku Leeds united wakihitaji kiasi cha Euro milioni 60 kufanya biashara.
Mpango huo umekuja baada ya West ham kuhitaji dau la Euro milioni 100 kumuachia Rice kiasi ambacho Man utd wanaona hawako tayari kukitoa,hivyo kumgeukia Muingereza mwezake Phillips anayefananishwa na gwiji wa zamani wa Italia Andrea Pirlo kutokana  na uchezaji wake.