Kiungo wa manchester united Paul Pogba amezua balaa klabuni hapo baada ya uongozi kuamua kuweka dau la Paundi 180m kwa timu ambayo itamuhitaji staa huyo.
Imeripotiwa kuwa united imeweka dau hilo ili kuzuia dili la mchezaji huyo kujiunga na Real madrid na Juventus ambazo zinamnyemelea kwa kasi mfaransa huyo.
Pogba 26 tayari amesharipoti katika kambi ya mazoezi ya klabu hiyo iliyopo barani asia kujindaa na msimu mpya wa ligi kuu nchini humo ambapo msimu uliopita timu hiyo ilikosa nafasi ya kumaliza nne bora na kushindwa kupata nafasi ya kushiriki michuano ya klabu bingwa barani ulaya.