Hatimaye kiungo wa Manchester United Paul Labile Pogba amesema hafurahishwi na maisha yanayoendelea kwenye klabu ya Manchester ya kupewa nafasi ndogo hivyo huenda akaamua kuondoka kwenye klabu hiyo kutokana na kupitia wakati mugumu zaidi kwenye maisha yake ya soka kuliko wakati mwingine wowote.
Pogba licha ya kusema hivyo tayari ameonyesha dalili zote za kutoridhika na maisha ndani ya timu hiyo huku akidaiwa yupo tayari kujiunga na Real Madrid ama kwenda nchini Italia kunako klabu yake ya zamani Juventus.