Home Soka Ronaldo aibeba Man Utd,Barca hoi tena usiku wa Ulaya

Ronaldo aibeba Man Utd,Barca hoi tena usiku wa Ulaya

by Dennis Msotwa
0 comments

Ni Cristiano Ronaldo tena unaweza kusema hivyo baada ya mshambuliaji huyo kuiwezesha timu yake ya Manchester United kuibuka na ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Manyambizi wa njano Villareal katika usiku wa mabingwa Barani Ulaya.

Villarel ndio walikuwa wa kwanza kupata goli dakika ya 53 kupitia kwa staraika Paco Alcacer akiunganisha vyema krosi ya Danjuma,Man Utd walichomoa bao hila dakika ya 60 kupitia kwa Alex Telles kwa bao safi la nje ya box akiunganisha mpira wa adhabu uliopigwa na Bruno Fernandes.

  Zikiwa imesalia dakika moja kati ya tano za nyongeza Ronaldo aliwapa pointi 3 muhimu kwa shuti kali lililomshinda golikipa wa Villareal Rulli na kuibua shangwe kwa mashabiki waliohudhuria katika dimba la Old Trafford.

banner

Kwa upande wa Barcelona wameendelea na mwanzo mbaya katika michuano hiyo kwa kipigo cha pili mfululizo baada ya kupokea kipigo cha mabao 3-0 kutoka kwa Benfica katika mchezo wa kundi E.

Matokeo mengine kwenye michezo ya jana ni kama ifuatavyo;

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited