Simu moja tu ya Sir Alex Ferguson imebadili uelekeo wa Cristiano Ronaldo aliyekua mbioni kuelekea Manchester City kujiunga na klabu hiyo na kuamua kujiunga na Manchester United iliyochini ya Olle Gunnar Solskjaer huku akiungana na mastaa kama Paul Pogba na Bruno Fernandes pamoja na Edson Cavani.
Awali Ronaldo alionyesha nia ya kuondoka Juventus ambayo ilihitaji paundi milioni 30 kumuachia staa huyo ambaye naye alikubali kujiunga na Man City iliyoonyesha nia ya kumsajili mshambuliaji huyo mwenye miaka 36 huku ikimuandalia mshahara wa paundi laki tano kwa wiki lakini kuingia kwa Man united kwenye dili hilo dakika za mwishoni kulibadilisha upepo na staa huyo sasa atatua Man United baada ya kukubali mapendekezo ya mkataba wa Man united ambao pia watailipa Juventus kiasi cha paundi 25 milioni.
Inadaiwa Ronaldo amekubali mshahara wa kiasi cha paundi 375000 kwa wiki akiacha mshahara mnono ambao angelipwa na Man city huku ikidaiwa simu ya Ferguson kwa mama wa mchezaji huyo ilibadili kila kitu na kumfanya staa huyo arudi Man united alipoondoka miaka 12 iliyopita ambapo alidumu klabuni hapo kwa miaka 6 akishinda mataji mbalimbali ikiwemo Epl mara tatu.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Man united inasemekana ina mpango wa kuwatoa kwa mkopo Anthony Martial kwenda Real Madrid ambayo itamlipa mshahara wote pamoja na Jesse Lingard kwenda Westham United ili kufidia kiasi cha mshahara wa Ronaldo klabuni hapo.